Breaking




Thursday 5 October 2017

HISPANIA YAKATAA WITO WA CATALONIA

Sungo blog

Serikali ya Hispania imeukataa wito uliotolewa na kiongozi wa Catalonia, Carles Puigdemont kuwepo kwa mapatano juu ya matakwa ya uhuru wa jimbo hilo.

Ofisi ya Waziri mkuu Mariano Rajoy, imesema Madrid haitokubali kusalitiwa na hivyo hakutakuwa na mazungumzo mpaka pale kiongozi huyo wa Catalonia atakapoachana na madai yake ya kampeni zisizo halali za kudai uhuru.

Awali Carles Puigdemont aliikosoa hotuba aliyoitoa Mfalme Felipe wa Hispania, ambaye aliiita kura ya maoni juu ya uhuru wa jimbo hilo, iliyofanyika siku ya Jumapili kuwa ni tendo lisilo ruhusiwa la kisaliti.

Mgogoro huo wa Catalonia umepiga soko la Hisa la Hispania siku ya Jumatano na kuonekana anguko lake la siku katika kipindi cha miezi 15.

Serikali ya Catalonia imesema kutakuwa na kikao maalumu cha bunge siku ya Jumatatu kuzungumzia matokeo ya zoezi la kura hiyo ya maoni, lililokumbwa na mgawanyiko.

No comments:

Post a Comment