Breaking




Tuesday, 17 October 2017

HIZI NDIZO REKODI ZA AJIB NA NIYONZIMA,JE NANI MKALI?

Sungo blog


Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajib ni wachezaji waliozungumzwa sana wakati wa dirisha la usajili kabla ya kuanza kwa msimu huu kwa sababu ya kuhama kutoka klabu zao na kujiunga na mahasimu wa klabu walizozihama.

Inatajwa kwamba Ajib alisajiliwa na Yanga kwa Tsh. 50 Mil pamoja na gari ndogo ya kutembelea (Toyota Brevis). Wakati huo ikielezwa Niyonzima ndiye mchezaji ghali kusajiliwa msimu huu baada ya kuvuta mtonyo unaokadiriwa kufika Tsh. 120 Mil.

Baada ya ligi kuanza Ajib ameshafunga magoli matatu na ku-assist moja katika mechi sita alizocheza wakati Niyonzima bado hajafunga wala kutoa assist katika magoli 14 ambayo Simba imefunga hadi dasa.

Unatabiri nani atafanya vizuri hadi mwisho wa msimu huu kati ya Niyonzima au Ajib?




No comments:

Post a Comment