Breaking




Monday 9 October 2017

JESHI LA POLISI KUMSHUGHULIKIA MANGE KIMAMBI

Sungo blog



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro amesema jeshi lake linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwanadada Mange Kimambi na linashughulikia suala hilo .

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa IGP Sirro amesema jeshi hilo linatambua uvunjifu wa sheria ya makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwadada huyo maarufu mitandaoni ikiwemo kutoa machapisho mbalimbali ya matusi na kashfa kwa serikali na viongozi wake lakini kwa sasa hawezi kusema ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mwadada huyo anayeishi nje ya nchi.

 

Aidha IGP.Sirro amesema Jeshi hilo halitawavumilia maafisa wa polisi na askari wanaowasaidia watu wanaofanya unyanyasaji kwa watoto kwa kuwafanyia vitendo vya ubakaji na ulawiti ili kukwepa mkono wa sheria huku akiwataka wananchi wanaohisi kutotendewa haki katika kushughulikia makosa ya aina hiyo kupeleke malalamiko kwa wakuu wa mikoa na viongozi wengine.

No comments:

Post a Comment