Breaking




Monday 9 October 2017

LEMA AMVIMBIA IGP SIRRO


Sungo blog

 Baada ya IGP Simon Sirro kutoa tamko la kusitisha mjadala juu ya shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na badala yake viache vyombo vya usalama viendelee kufanya kazi hiyo, Mbunge wa Arusha Mjini amejibu kauli hiyo kwa kuipinga na kumuahidi kuwa wataendelea na majadiliano

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amejibu IGP Sirro kwamba wao wataendelea kujadili suala la Lissu kwa nguvu na bila kumuogopa mtu yeyoote

"IGP Sirro, Tutaendelea kujadili swala la Mh. Lissu kwa nguvu zote bila kumuogopa mtu yeyote. Utu na kweli una maana zaidi ya cheo na mshahara" Lema.

Akiwa ziarani Jijini Mbeya IGP Simon Sirro alitaka mjadala kuhusu kupigwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ufungwe mara moja wakati alipokuwa akizungumza na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo amewaonya wanasiasa kuacha kuuendeleza na waliachie jeshi lifanye kazi yake.

Hata hivyo kauli ya IGP kutaka mjadala wa Lissu ufungwe umeibua hoja kutoka kwa watu mbalimbali akiwepo Wakili Peter Kibatala ambaye yeye ameahidi kutumia uwezo wake kwenye sheria kuhakikisha kauli ya IGP Sirro inatenguliwa.



No comments:

Post a Comment