Sungo blog
Na.Ahmad Mmow.
MAKATIBU tawala wa mikoa(RAS's) nchini wameagizwa kufuatilia, kusimamia na kuhakikisha wauguzi wanalipwa madai yao yote yanayotokana na kazi walizofanya nje ya muda uliopo kisheria.
Agizo hilo limetolewa leo na waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa(MB) alipozungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa wauguzi na kongamano la kisayansi uliofanyika leo katika manispaa ya Lindi.
Waziri mkuu Majaliwa ambae alikuwa mgeni rasimi kwenye mkutano huo wa 45 ambao uliandaliwa na chama cha wauguzi nchini(TANNA), alisema kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu madai hayo kutoka kwa wanataaluma hao muhimu kwa afya na uhai wa binadamu.Hivyo kuna umuhimu mkubwa wa madai hayo kulipwa.Huku akiwataka makatibu tawala hao kuhakikisha hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu kusisikike tena wauguzi wanaendelea kudai malipo hayo.
Alisema mamlaka husika, ikiwamo wakurugenzi wa halmashauri nchini wahakikishe malipo ya muda wa ziada yanatengwa na kulipwa kwa wakati.Huku akisisitiza kwa kusema ;
" Malipo hayo yapewe kipaumbele,lazima walipwe nasio vinginevyo,"alisema Majaliwa.
Katika hali inayoonesha serikali imedhamiria madai hayo yalipwe,waziri Majaliwa amemtaka mwenyekiti wa chama cha wauguzi nchini, Paul Magesa kufuatilia kwa karibu zoezi hilo.Huku akimtaka kumjulisha iwapo kutakuwa na vikwazo vitakavyojitokeza katika utekelezaji wa agizo hilo.
Mbali na agizo hilo kwa makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri nchini,waziri mkuu ameonya tabia za baadhi ya viongozi wa serikali kutumia madaraka yao vibaya kwa kuwaweka rumande watumishi wa sekta ya afya bila kufuata taratibu,kanuni na sheria.
Kuhusiana hilo ameitaka wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kufutilia kwa karibu taarifa za vitendo hivyo.Ili watakao bainika kutenda wachukuliwe hatua za kinidhamu haraka.
Majaliwa alisema taaluma za uuguzi na udaktari zinamisingi na taratibu zake ambazo zinatakiwa kufuatwa na kuheshimiwa. Hivyo yeyote ambae hataki kuziheshimu taratibu hizo hanabudi kuchukuliwa hatua
"Viongozi lazima wazingatie sheria,kanuni na taratibu.Yapo mabaraza yanaouwezo wakubaini ukubwa wakosa,nihatua gani zichukuliwe na nani wanapaswa kuchukua hatua.Kwahiyo mabaraza yashirikishwe na yatumike ili yatambue hatua zinachukuliwa kwa watumishi hao kwenye maeneo yake,"alisisitiza Majaliwa.
Aidha alitoa wito kwa wauguzi kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia viapo vya kazi hiyo.Ikiwamo kuepuka lugha chafu na kali kwa wagonjwa,rushwa na dharau
No comments:
Post a Comment