Sungo blog
Ofisi ya takwimu ya taifa wametoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei kwa mwezi septemba 2017 kwa kipimo cha mwezi kuonyesha kwamba umepanda ukilinganisha mwezi uliopita.
Mkurugenzi mkuu wa wa sensa ya watu na jamii Ephaim Kwesigabo ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokua akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa mfumuko wa bei kwa mwezi septemba kwa kipimo cha mwezi umeongezeko kwa 00.2 ikilinganisha na kupungua kwa aslimia 0.4 mwezi Agosti mwaka huu.
Aidha amesema kuwa fasihi za bei zimeongezeka hadi 108.48 mwezi huu kutoka agosti. Hivyo ongezeko hili limetokana na kupanda bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.
Baadhi ya bidhaa zilizochangia ongezeko la fasihi ni pamoja na dagaa kwa asilimia 7.5, nazi 3.1, viazi vitamu 3.0, mchele 1.5 na ndizi 1.5. Pia kwa bizaa zisizo za chakula ni mkaa kwa asilimia 4.0 dizeli 2.4 na petroli 0.6.
Hivyo kupelekea kuongeseka kwa asilimia katika mwezi huu.
No comments:
Post a Comment