Breaking




Saturday 7 October 2017

TAARIFA KUHUSU DONALD NGOMA KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA

Sungo blog



Wakati Yanga ikiendelea kuwa na wakati mgumu tangu kuanza kwa msimu wa 2017/18, taarifa za kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Donald Ngoma anaweza kuukosa mchezo dhidi ya Simbe zimeshika kasi.

Ngoma aliumia katika mchezo dhidi ya Mtibwa wiki iliyopita ambapo alishindwa kuendelea na mchezo kipindi cha pili kukawa na hofu kubwa kuwa anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu huku ikijulikana Yanga watakutana na wapinzani wao wa jadi, Simba mnamo Oktoba 28 mwaka huu.

Akizungumza maendelea ya mshambuliaji huyo,
Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema ni kweli afya ya Ngoma haikuwa sawa lakini bado wanasubiri ripoti ya daktari kwa kuwa awali alipewa wiki moja ya kupumzika.

Wiki ambayo mchezaji huyo amepumzikia ndipo ambapo kuna mapumziko mafupi ya Ligi  Kuu ya Vodacom kutokana nakupisha michezo ya kimataida.

“Siyo kweli kuhusu hizo taarifa, Ngoma kweli afya yake haikuwa sawa lakini kwa sasa tunaendelea kusubiri ripoti kamili ya afya yake,” Ten.

No comments:

Post a Comment