Breaking




Thursday 5 October 2017

TAIFA STARS YASHINDWA KUFANYA MAZOEZI

Sungo blog


 

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars haijafanya mazoezi jioni ya leo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuwapa wachezaji mapumziko.

Kikosi hicho ambacho amabcho kinaundwa na mastaa wengi wanaocheza soka nje wakiwemo Simon Msuva na Mbwana Samatta kilifanya mazoezi jana lakini leo asubuhi walifanya kidogo kisha jioni wakabadilisha program na hawakufika kwenye mazoezi ya uwanjani.

Jana walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani nje kidogo mwa Jiji la Dar lakini leo waliendelea na program zingine.

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika jana jioni kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 12, Kocha wa Stars, Salum Mayanga alikuwa akiwakazania washambuliaji wake kuhakikisha wanakuwa imara katika kufumania nyavu zaidi, ambapo alikigawa kikosi makundi mawili.

Katika mazoezi hayo ambayo Stars inajiandaa na Malawi kulionekana kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na jinsi wachezaji walivyokuwa wakijituma uwanjani kuhakikisha wanafanya vyema katika mchezo huo wa Jumamosi.

No comments:

Post a Comment