Breaking




Monday, 2 October 2017

‘Ugonjwa wa kimeta unaathiri hadi binadamu’ – Wizara ya Kilimo








    

Sungoblog

Serikali imeanza mkakati wa kutoa  chanjo ya mifugo ili kukabiliana  na mlipuko wa ugonjwa wa kimeta (Anthrax) unaoonekana kuathiri  zaidi mifugo na wanyama pori  na baadae kuenea kwa binadamu.

Mratibu wa afya kutoka Wizara ya Afya, Juvilet Bernald amesema ugonjwa  wa kimeta umekuwa tatizo zaidi kwenye ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania ikiwemo Ngorongoro na Monduli ambapo wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakipata maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuwa wamekua wakila nyama za mifugo hiyo ikiwa imekufa.

Kwa upande wake Dr. Bedan Masuruli kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,ambaye pia ni msajili wa baraza la vetenary,alisema tatizo la kimeta ni kubwa kwa sababu linaathiri pia binadamu na hivyo aliongeza kuwa ipo haja kwa wataalamu kuunganisha nguvu na kutoa elimu kwa maeneo yanayoathiriwa zaidi na ugonjwa huo

No comments:

Post a Comment