Breaking




Thursday, 26 October 2017

WANANCHI WAENDELEA KUPIGA KURA KE


Sungo blog

Wananchi nchini Kenya leo wanapiga kurakwenye uchaguzi wa marudio wa raisbaadaya matokeo yake kufutwa na mahakamaSeptemba 1, mwaka huu.

Uchaguzi huo ambao umegubikwa na vurugumbali mbali kwa baadhi ya maeneo,unaendelea huku kukiwa na mvua kubwa nakuleta kikwazo kwa baadhi ya maeneokwenda kupiga kura.

Katika baadhi ya maeneo ikiwemo Kiberaambayo ni kambi kubwa ya NASA, yamekuwana vurugu kwa kujaribu kukwamisha zoezihilo la upigaji kura, kwa kufunga njia zakwenda kwenye vituo vya kupigia kura,kitendo kilichopelekea polisi kuingilia kati nakuzifungua njia hizopamoja na kupigamabomu ya machozi ili kutuliza ghasia.

Maeneo mengine yameonekana kufurika watu na kuendelea na zoezi la kupiga kura, licha ya changamoto hiyo kubwa ya mvua, ambayo pia imepelekea kukwama kwa baadhi ya magari yaliyokuwa yakisafirisha vifaa vya kupigia kura.

Katika eneo la Garisa askari polisi mmoja amefariki na wengine watatu kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakitumia kusafirisha makaratasi ya kupiia kura kupata ajali.

No comments:

Post a Comment