Breaking




Monday 9 October 2017

YANGA IMETOKA BILABILA NA KMC INAYOSHIRIKI LIGI DARAJA LA KWANZA

Sungo blog


 

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Dar Young Africans ,leo walikua uwanjani kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya KMC(Kinondoni Municipal Council) inayoshiriki ligi daraja la Kwanza.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Azam Complex-Chamazi majira ya saa moja jioni umemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Vijana wa KMC wanaonolewa na Felix minziro walionekana kujiamini zaidi upande wa ulinzi na kuweza kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga.

Awali uongozi wa Yanga ulisema mapato ya mchezo huo yatatumika kukarabati uwanja wa Kaunda ambao unamilikiwa na klabu hiyo uliopo pale Jangwani

No comments:

Post a Comment