Sungo blog
Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amemjia juu katibu wa halmashauri kuu ya taifa ya ccm itikadi na uenezi Humphrey Polepole akimtaka kuacha ubinafsi na kujimilikisha chama cha mapinduzi.
Hii imekuja baada ya Polepole kuonyesha kutokuwa na utayari wa kumpokea msanii maarufu Wema Sepetu aliyetangaza kuhamia chama cha mapinduzi jioni ya leo akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
"Hiki chama hujakiunda wewe,umekikuta kama tulivyokikuta sis,kina waasisi wenye uchungu nacho na wako kimya,wewe ni nani mpaka uwakatishe watu moyo wa kukitumikia chama hiki kama vile ndo unakimiliki"Amehoji Steve Nyerere akimuuliza Polepole.
Msanii huyo amemuonya Polepole aache ubinafsi kwenye kukitumikia na kukijenga chama
"Hiki chama hujakiunda wewe wala kukianzisha wewe, umekikuta kama tulivyokikuta wote, kina waasisi wenye uchungu nacho na wako kimya, wewe ni nani ukatishe watu moyo kukitumikia kama vile ndio unakimiliki, tulia polepole chama cha wote hiki. Usilete ubinafsi kwenye kutumikia na kujenga ngome, hatuhitaji wenye cement na nondo tu, acha hata mwenye jiwe lake aweke kikubwa nyumba isimame. Ni mchango pia.". Ameandika Steve Nyerere akiwa ameambatanisha picha ya Hurmprey Polepole.
Polepole alimtaka wema sepetu ajitathmini upya hazma yake ya kurejea CCM na ikiwezekana abaki hukohuko CHADEMA kwani CCM siyo daladala kwamba mtu anaweza kupanda na kushuka wakati atakao.







No comments:
Post a Comment