Saturday, 23 December 2017

RASMI ASANTE KWASI MALI YA SIMBA

Sungo blog


Beki wa kimataifa wa Ghana, Asante Kwasi sasa ni ruksa kuichezea klabu ya Simba baada ya klabu hiyo ya Msimbazi kumalizana na Lipuli fc.

Kabla ya klabu hizo kuafikiana, klabu ya Lipuli ambayo ilikua waajiri wa Kwasi waliwasilisha malalamiko kunako Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikidai kuwa Simba ilikuwa ikifanya njama za kumsajili beki huyo Kinyemela.

Mwenyekiti wa Lipuli, Ramadhani Mahano  amesema kuwa wameruhusu Kwasi kutua Simba baada ya klabu hizo kukaa mezani.

Alisema tayari wamemkabidhi Kwasi barua ya kumruhusu kuchezea Simba baada ya kukamilishwa kwa taratibu zote za uhamisho kutoka kwao.

“Ni kweli tumewapa simba barua ya kumtumia Kwasi, wanaweza kumtumia katika michezo yao,hii ni baada ya kukamilisha taratibu za uhamisho wa wachezaji wa klabu za ligi kuu kama ilivyoainishwa kwenye kanuni.”

“Tumemruhusu baada ya Simba kutulipa millioni 25 kuanzia hapa tunapozungumza Kwasi ni mali ya Sima.”

No comments:

Post a Comment