Breaking




Friday, 23 February 2018

DC ZAINAB: "MSINICHUKULIE POA,NILIHIFADHI QURAAN JUZUU 30 NIKIWA NA MIAKA 15"

Sungo blog


 

 

Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Zainab Abdalah ziku mbili tatu hivi  alionekana kwenye "head lines" kutokana na ujumbe wake wa kumshukuru mume wake kwa kukubari ushauri wake wa kuoa mke wa pili.


Ujumbe huo uliibua hisia nyingi , kuna ambao walimpongeza kwa ujasiri huo lakini wengine walimsema vibaya.

Bi Zainab ameibuka tena kuwajibu wale ambao walimsema vibaya kwa kuwafahamisha kuwa yeye ana ufamu wa kutosha juu ya elimu ya dini ya kiislamu ,hivyo amefanya hivo kwa mujibu wa mafundisho ya dini.

kupitia ukurasa wake wa Instagram DC zainab ameeleza kuwa alihifadhi Quraan juzuu 30 akiwa na umri wa miaka15,alihifadhi hadithi elfu moja (1000) za Mtume (s.a.w) akiwa na umri wa miaka mitatu tu.

Pia  amekuwa bingwa wa mashindano ya Quran Afrika Mashariki na kati, Mashindano ya Quran Zanzibar na Mashindano ya Quran Libya,ameshawahi kuhifadhisha vijana wengine Quran ndani na nje ya Tanzania,ameshawahi kuwa Jaji kwenye mashindano ya Quran.

 Ujumbe ufuatao ameuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram

 "Zainab ambaye watu wengi hawamfaham..
1. Nilifanikiwa kuhifadhi hadithi elfu moja (1000) za Mtume (s.a.w) nikiwa na umri wa miaka mitatu tu.
2. Nimehifadhi Quran Juzuu 30 nikiwa na umri wa miaka 15 tu.
3. Nimekuwa bingwa wa mashindano ya Quran Afrika Mashariki na kati, Mashindano ya Quran Zanzibar, Mashindano ya Quran Libya.
4. Nimeshawahi kuhifadhisha vijana wengine Quran ndani na nje ya Tanzania.
5. Nimeshawahi kuwa Jaji kwenye mashindano ya Quran.

Ahlul Quran wa Sunnah. 
M/Mungu atupe husnul khatimah!"
JUMAA KAREEM🕌🌙

No comments:

Post a Comment