Sungo blog
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasilianoya klabu ya Simba, Haji Manara ametoa witokwa mashabiki, wapenzi na wanachama watimu hiyo kuacha kuwazomea hasimu waoYanga SC katika mchezo wao wa klabubingwa Afrika raundi ya kwanza watakaocheza dhidi ya St Lous ya Seychelles.
Haji Manara ameyasema hayo kupitia kikaochake na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam.
“Natoa wito kwa washabiki wa Simba watakaoenda uwanjani kwenye mechi ya Yanga siku ya Jumamosi wasiizomee, tuzomeane kwenye ligi ya nyumbani..cc sote ni watanzania na tunawakilisha nchi,”amesema Manara.
Haji Manara ameyasema hayo wakati ambao timu ya Simba SC nayo ikikabiliwa na kibarua kizito siku ya Jumapili ambapo itaivaa Gendarmerie Nationale FC ya Djibouti.







No comments:
Post a Comment