Sungo blog
Taifa la Korea Kaskazini linatarajiwa kuandaamaadhimisho ya 70 ya gwaride la jeshi lakekabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpikiya majira ya baridi nchini Korea Kusini.
Gwaride la kila mwaka la Pyongyanglinaloadhimisha kuanzishwa kwa jeshi laKorea Kaskazini limekuwa likifanywa kilamwezi Aprili kwa kipindi cha miaka 40.
Hatahivyo vyombo vya habari nchini humovilitangaza mapema mwaka huu kwambatarehe ya kufanyika kwa gwaride hilo lakijeshi imebadilishwa hadi Februari 8.
Korea Kaskazini imepuuzilia mbali ukosoajiwa mpango wake ikisema kuwa hakuna mtualiye na uwezo wa kuishutumu.
''Ni utamaduni na swala muhimu sanakwamba kila taifa duniani linasherehekeauzinduzi wa jeshi lake' , kilisema chamatawala cha wafanyikazi Rodong Sinmun.
Marekani imesema kuwa ingependeleagwaride hilo kutofanyika kwa kuwa kwa sasawatu wanalenga michezo ya Olimpiki.
Siku ya Alhamisi, Korea Kaskazini ilisemakuwa haina mpango wa kukutana na maafisawa Marekani , kulingana na chombo chahabari nchini Korea Kaskazini KCNA.
Serikali ya Korea Kusini imesema kuwamwezi uliopita kwamba wanajeshi 13,000 navifaa 200 vilipatikana karibu na uwanja wandege wa Pyongyang katika kilekinachoonekana kuwa gwaride la majaribio.
''Kile tunachotarajiwa kuona katika gwaride hilo la kijeshi ni magari ya kubeba silaha, idadi yake na iwapo yanabeba silaha mpya'' , alisema David Schmerler, mchanganuzi wa Korea Kaskazini katika kituo cha James Martin cha masomo ya kuzuia kusambaa kwasilaha







No comments:
Post a Comment