Breaking




Thursday, 8 February 2018

MAGEREZA WATAJA SABABU ZA KUMZUI PROFESA JAY KUMUONA SUGU GE


sungoblog

Mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro, Joseph Haule ‘Profesa Jay’  jana alizuiwakumuona mbunge wa Mbeya Mjini, JosephMbilinyi pamoja na katibu wa ChademaKanda ya Nyanda za Juu Kusini, EmmanuelMasonga baada ya kuzuiwa na maofisa wamagereza.

Profesa Jay aliyeambatana na mke wake, Grace Haule walifika jana jijini Mbeya nakwenda gerezani kuwaona Sugu na Masongaambao wapo mahabusu wakikabiliwa na kesiya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya RaisJohn Magufuli.

Mkuu wa magereza Mkoa wa Mbeya,Kamshina Msaidizi Mwandamizi (SACP), PaulKijida alisema walimzuia Profesa Jay kwasababu haikuwa siku ya kuwaona mahabusu.

‘Kweli amekuja hadi ofisini kwangulakinitaratibu hazipo hivyoSiku za kawaida kamahizi tunamruhusu mtu anayempelekea chakulaau ataruhusiwa pale mfungwa au mahabusuanaumwa au mwanasheria wake anaruhusiwakama tu kuna kitu muhimu’’ alisema Kijida nakuongeza kwamba

‘’Lakini tukisema kila mtu kwa muda na sikuanayotaka iwe siku ya kuwaona wafungwa au mahabusu hatutafanya kazi sasa. Siku za kuwaona wafungwa na mahabusu kwa watu wa kawaida ni Jumamosi na Jumapili tu,” alisema mkuu huyo wa magereza.

‘’Nimejaribu kuonana na RPO (mkuu wa magereza mkoa) lakini naye ameonekana kusita kunipa kibali cha mimi kuonana nao. 

"Na inaonyesha kuna kitu nyuma kimejificha. Lakini nimefunga safari kuja kuonana nao hivyo siwezi kuondoka bila kuonana hivyo kesho(leo) nitakuwepo mahakamani, nitazungumza nao,” alisema Profesa Jay jana.

Alisema anachotambua ni kuwa mbunge hazuiliwi kuwaona mahabusu gerezani, lakini jambo hilo limemshangaza.

Akizungumza na mama yake Sugu aitwaye Desderia, alimtaka kuwa na ustahimilivu katika kipindi hiki ambacho mwanaye yupo kwenye misukosuko.

Profesa Jay alisema, “mama usihofu, yule hajabaka wala hajaiba bali kilichomuweka ndani ni kutetea masilahi ya wananchi. Na ndio maana hata sisi tumeacha kazi zote huko kuja kuhakikisha tunashughulikia jambo hilo na naamini haki itatendeka tu. 

"Na hapa usione tupo wachache kuja hapa nyumbani, lakini Sugu ana kundi kubwa sana la watu na tumegawana majukumu ya kufanya kuhusu hili tatizo.”

No comments:

Post a Comment