Breaking




Thursday, 15 February 2018

TANZANIA YAPATA MSAADA WA MABILIONI KUTOKA EU


sungo blog


Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia serikali ya Tanzania msaada wa Euro Milioni 4.5 (Tsh. 12 Bilioniili kufanikisha miradi mikubwamitatu ya sekta ya kilimo ambayoinatekelezwa kupitia Mpango wa KuendelezaKilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

Miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa yaIringaMorogoro ambapo itafanyika miradimiwili.

Akizungumza kuhusu msaada huoNaibuWaziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa alisemamsaada huo utasaidia wakulima wadogokuboresha kilimo chao na kuwa chakibiashara zaidi kuliko sasa.

Mwanjelwa alisema pamoja na kuwanufaishawakulima, pia kama nchi itanufaika kutokanana biashara itakayokuwa ikifanyika jamboambalo litasaidia uchumi wa nchi kukua.

“Wamekusudia kufufua kilimo cha kisasa, kilimo bora ili Watanzania wanufaike na kilimo kwa kuwa na soko. Faida yake ni upatikanaji wa chakula, lishe na biashara na mwisho wa siku wananchi wote wanufaike,” alisema Mwanjelwa.

Kwa upande wa Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Roeland Van de Geer alisema EU imedhamiia kusaidia mirad mingi hapa nchini katika sekta ya chakula ili kuhakikisha kuwa jamii ya Tanzania inakuwa na chakula cha kutosha.

No comments:

Post a Comment