Breaking




Thursday, 22 February 2018

ZITTO KABWE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MOROGORO

Sungo blog

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi cha Mgeta wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mahojiano. 

Zitto yupo katika ziara ya mikoa mbalimbali kwa ajili ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama hicho. 

Katibu Kamati ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma  wa ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema mpaka sasa bado yupo anashikiliwa na Polisi hawajui ni kosa gani ambalo Zitto Kabwe limefanya akamatwe 

Nae Wakili wa Zitto Kabwe, Emmanuel Lazarus Mvula amesema jalada la mashataka dhidi yake limefunguliwa katika kituo cha Polisi Mgeta. 

No comments:

Post a Comment