Breaking




Tuesday 13 March 2018

AFUKUZWA KAZI BAADA YA KUMTEMEA MATE SHABIKI

Sungo blog


Nyota wa zamani wa Liverpool na Mchambuzi wa Soka katika kituo cha Sky Sports, Jammie Carragher, amesimamishwa kazi kwa muda kutokana na kitendo cha kumtemea mate binti ambaye ni shabiki wa Manchester United.

Carragher alifanya tukio hilo mapema baada ya mchezo uliowakutanisha Manchester United dhidi ya Liverpool wakati akitoka kukava habari kuhusiana na mchezo huo.

Kwa mujibu wa Sky Sports TV, Msemaji wa kituo hicho amesema Carragher hatokuwepo kazini kwa takribani wiki moja inayokuja, na baadaye watakuja kutoa hatma ya mchezaji huyo kama ataendelea kusalia kazini au kuondoshwa kabisa.

Kufuatia kitendo hico, Carragher tayari alikuwa ameshaomba msamaha kwa binti huyo mwenye miaka 14 na msamaha wake ulipokelewa.

No comments:

Post a Comment