Breaking




Friday 2 March 2018

‘Mama Nimemuona Daddy Joseph anapelekwa Jela’ Mtoto wa Sugu

Muigizaji wa Bongo movie ambaye pia ni mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya mjini Sugu, Faiza Ally ameeleza machungu yake baada ya mtoto wake kulia baada ya Baba yake kufungwa jela miezi mitano.
Siku chache zilizopita Mbunge wa Mbeya mjini kupitia tiketi ya CHADEMA Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha ya fedheha dhidi Rais Magufuli.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza amesema kuna baadhi ya vitu ambavyo vilimfanya akose huruma na Sugu lakini mtoto wake Sasha alimfanya ajisikie vibaya alipomhadithia kuwa kamuona Baba yake akienda jela.
“Hivyo ni baadhi ya vitu tu ambavyo vinavyo nifanya nikose huruma nae lkn jana sasha alienda dukani na dada akaja kuniambia MAMA NIME MUONA DADDY JOSEPH KWENYE GAZETI ANAPELEKWA JELA ndio nikajisikia vibaya sana,” -Faiza
“Nikahisi nimekua mtu mbaya sana na mkatili kumtakia baba Sasha matatizo nilijaribu kuongea na mwanangu na kuona kweli uchungu una badilisha watu , asili yangu sio ubaya lkn uchungu umenifanya nisijali na nifurahie lililo tokea nimeona kama ni wkt wake na yeye wa kukutwa na majanga,” -Faiza
“Nimekosa raha sana na nimeamua kuandika haya kujiridhisha lkn napigana na akili yangu na moyo akili inajua kuwa ni Natural feelings kwa binaadamu lkn moyo unakataa unasema huyu sio mimi lkn sasa naamini usemi unao sema uchungu una badilisha watu.” -Faiza

VIDEOChangamoto Zinazo Wakabili Wakulima Juu Ya Wafugaji Kijiji Cha Zinga.

No comments:

Post a Comment