Breaking




Friday 2 March 2018

MATAPELI WA BIMA WAPEWA ONYO KALI

Sungo blog


Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA)imetoa onyo kali kwa watu wanaowatapeliwananchi kwa kuwauzia bima za kugushi nahivyo kuwasababishia hasara na kuikoseshaSerikali mapato,Matapeli hao ambao wengiwao hawana leseni za kufanya biashara yaBima wametakiwa kuacha mara moja wizihuo kwani mkono wa sheria unawasaka ilihatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidiyao.

Akizungumza wakati wa zoezi la ukaguzi wabima katika Vyombo vya moto lililofanyikaMjini Dodoma ,Bibi Stella Guli Rutaguzaamesema jumla ya magari 586 yalifanyiwaukaguziambapo  wamebaini  magari 25,pikipiki za miguu mitatu 5(bajajpikipiki zamiguu miwili 2 yakiwa na Bima za kugushi huku magari mengine 19 yakiwa hayana bima.

 Rutaguza amesema kuwa wamefaminikiwa kuwakamata watu Wawili ambao wanatuhumiwa kujihusisha na kuuza bima za kugushi kwa wananchi na tayari wako mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Bibi Stella Rutaguza amesema zoezi la kuwasaka watu wanaouza bima feki kwa na kuwaibia wananchi na Serikali ni endelevu hapa Dodoma na Nchi nzima kwa ujumla.

"Tunataka kukomesha tabia hii chafu kwenye Soko la Bima", hivyo tunawataka vishoka wa Bima popote walipo watafute kazi halali ya kufanya maana Mamlaka ya Usimamizi wa Bima haitawafumbia macho na mkono wa sheria hawataukwepa", alisema Rutaguza.

Amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya kutokuibiwa na matapeli hawa wa Bima kwa kununua Bima kwenye ofisi zilizosajiliwa na kupewa Leseni na Serikali kwa ajili ya kufanya biashara ya Bima na kuacha kununua Bima kiholela mitaani kwa watu wasiofahamika.

No comments:

Post a Comment