Breaking




Monday 12 March 2018

POLEPOLE AELEZA KWA NINI VIJANA WA MBEYA WANAFELI

Sungo blog

Katibu wa Itikadi na Uenezi  CCM Taifa, Ndg. Humphrey Polepole amesema sababu kubwa ya vijana wa Mbeya kuonekana kuyumba ni kutokana na kunyimwa nafasi za kuwa viongozi.

Akiwa Mkoani Mbeya kwenye ziara, Polepole ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wanachama wa CCM ambapo amesema kwamba watu wa Mbeya wamekuwa wakishindwa kuwapatia vijana uongozi ndiyo maana wameyumba kitu ambacho ni makosa kwani dunia nzima vijana wanapaswa kupewa uongozi.

Polepole amesema wao kama CCM wanataka kuwasaidia vijana hao kwa sababu ndicho chama ambacho ni sauti ya wanyonge, wasio na uwezo pamoja na wafanyabiashara ndogondogo

Aidha Polepole ameongeza kwamba "Tuchuke maoni yao tuielekeze serikali ikatatue na kisha tuiangalie serikali inafanya nini kisha tupeleke na kuzisema sifa za serikali  na kazi ambazo zinafanywa na serikali yetu. Wananchi watatupenda," Polepole.

Pamoja na hayo kiongozi huyo amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kinapaswa kuwa Chama kinachotoa majibu papo kwa hapo kwa wananchi wake.

No comments:

Post a Comment