Sungo blog
Jux.
NOVEMBA 3, 2016 mwanazuoni na mwandishi nguli duniani mwenye asili ya Nigeria, Wole Soyinka akiwa katika bustani ya kisasa ndani ya Chuo Kikuu cha Oxford cha nchini Uingereza alitoa ahadi ya kuiharibu kadi yake inayompa nafasi ya kuishi nchini Marekani (Green Card) endapo Donald Trump atakuwa rais wa Marekani.
Novemba 9, mwaka huo baada ya Trump kushinda urais wa Marekani, Wole ambaye ni Muafrika wa kwanza kutunukiwa tuzo ya heshima ya Nobel ya mwaka 1986, aliliambia Shirika la Habari la AFP kuwa ametimiza ahadi yake kwa kuiharibu kadi yake huku akijinasibu;
“Tayari nimeshafanya, nimetoka Marekani, nimefanya kile nilisema ningekifanya, nimetupa green card yangu, nimerudi penye ninastahili kuwa (Nigeria).”
Ukija Kibongobongo hili jambo halijakaa sawa! Wapo mastaa wengi ambao wamekuwa wakitoa ahadi mbele ya jamii lakini mwisho wa siku inakuwa ‘chenga’ ama feki.
Harmonize
Katika makala haya, inawachambua baadhi ya mastaa hao;
Ni mmoja kati ya ‘vichwa vikali’ kwenye Muziki wa R&B Bongo na pia mwenye heshima zake lakini katika harusi ya Mbongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ iliyofanyika usiku wa Januari 14, mwaka huu, Jux alitoa ahadi feki.
Katika usiku huo, Jux aliyeongozana na mwenza wake, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ alitoa ahadi ya kumlipia ada ya shule ya mwaka mzima mmoja wa mtoto wa Shilole kama namna ya kumpunguzia mwanadada huyo majukumu lakini hadi sasa imebaki stori tu.
Shilole alipotafutwa kuhusiana na ishu hiyo alibaki kuchengachenga akicheka tu kwa kuilinda heshima ya Jux.
Kama ilivyo kwa Jux kwenye harusi hiyo, Harmonize ambaye ni memba wa kwanza kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’ naye akiwa na mwandani wake aitwaye Sarah ambaye ni Mzungu, alitoa ahadi kwa Shilole ya kutoa shilingi milioni tisa ambayo ni thamani ya gari aina ya Noah ambapo alisema itamsaidia kusambaza chakula chake ‘Shishi Food’.
Alipotafutwa Shilole kuhusiana na hili nalo alichenga na mpaka sasa hakuna mazingira ya uwepo wa gari hilo nyumbani kwake.
Diamond.
Agosti 30, 2016, staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz akiwa nchini Marekani akitengeneza video ya Marry You alitumia ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka picha ya gari aina ya Rolls Royce na kuandika;
“Nataka nibadilishe aina ya gari sababu imekuwa ni muda mrefu, nafikiri ni muda wa kuwa na gari nililokuwa nalitamani siku zote, gari la ndoto yangu ni Rolls Royce na ndio ninalotaka kulinunua mwaka huu wa 2016 na litakuwa na jina la PLATNUMZ na sio namba za kawaida.”
Ndoto hizo zilikuja kuyeyuka, hadi sasa hakuna cha Rolls Royce wala ‘Rose Rozi’.
Rolls Royce ni magari yanayozalishwa na kampuni ya Uingereza na yalianzishwa na Charles Stewart Rolls na Sir Frederick Henry Royce, Machi 1906. Bei yake huanzia $300,000 (zaidi ya Mil. 670 za Kibongo) mpaka $500,000 (Bilioni 1).
AliKiba.
Unaweza kujiuliza ‘why’ King Kiba ameingia kwenye listi hii! Okey, mchana wa Septemba 24, 2016 mida ya saa nane kasoro, Kiba akiwa mgeni mualikwa katika Fainali za Shindano la Dance 100% zilizofanyika katika Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay Jijini Dar alitoa ahadi ya kuwachukua baadhi ya washindi wa shindano hilo na kufanya nao kazi.
Katika shindano hilo, Team Makorokocho lilibuka na ushindi na kujinyakulia kitita cha milioni 7.
Mpaka sasa hakuna wakali wowote wa Dance100% waliochukulia na Kiba katika kazi zake. Kuonesha hilo, katika Tamasha la Fiesta mwaka jana na shoo zake zote za ndani, Kiba amekuwa akionekana na dansa mmoja tu wa kike ambaye yupo naye kwa muda mrefu anayejulikana kwa jina la Jojo.
Nay wa Mitego.
Haaa haaa! Nay naye ameingia kwenye listi ya wazee wa ahadi feki. Februari 9, 2015 rapa huyu mw-enye sauti ya mk-wara, kati-ka moja ya maho-jiano na TV moja nchini alitoa ahadi feki kwa mashabiki wake.
Unajua alisemaje? Eti alitenga bajeti ya kama milioni 60 hivi ya kukamilisha kolabo yake na msanii mkubwa kutoka Nigeria ambaye alimficha jina.
Akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa, gharama hiyo itajumuisha gharama ya video chini ya Kampuni ya Godfather nchini afrika Kusini.
“Kolabo sio rahisi kama watu wanavyodhani, inatakiwa uwe na pesa za kutosha.
“Pia natakiwa kumsafirisha msanii kutoka Nigeria mpaka Sauz, anahitaji ‘treatment’ ya tiketi ya ndege nzuri, anahitaji hoteli nzuri, kwa hiyo ni gharama kubwa sana. Ni kama milioni 50 au 60 nadhani inaweza kutosha. Ukiangalia pia na mimi inanibidi nisafiri na timu yangu, kama sio watu wawili au watatu.”
Mpaka sasa miaka mitatu imekatika hana kolabo yoyote kimataifa hata ya nchi ya jirani hapo Kenya.
No comments:
Post a Comment