DAMASI Francis Damiano, aliyezaliwa 01 Jun 2001, ameshinda nafasi ya Tatu na kupata Medali ya Shaba kwenye Mbio ya wavulana (Boys 3000m) michuano ya sita ya dunia ya Vijana ya Jumuia ya Madola (Bahamas 2017 Commonwealth Youth Games) akitumia muda wa 8.37.51 wakipishana kwa sekunde 13.55 na Mshindi wa kwanza ambaye ni Mkenya na sekunde 2.36 na mshindi wa pili ambaye ni Mcanada.
Kwa kutwaa Medali hiyo, Damasi Francis ameiwezesha Tanzania kushika nafasi 19 kwenye ushindi wa jumla kwenye Riadhaa tukifungana na Botswana ,Cyprus, na South Africa huku tukichukua nafasi ya 31 kwa ushindi wa jumla wa michezo yote wa medali tukifungana na Nchi za Grenada, Namibia na Rwanda.
Hakika kuna fursa na nafasi zaidi za kunyakuwa Medali pale tutakapokuwa na chaguzi nzuri za washiriki wa Mashindano mbalimbali ya kimataifa na maandalizi mazuri.
No comments:
Post a Comment