HADITHI YA UTAJRI WA MZEE FISI. Sehemu ya 5.
Baada ya mzee fisi kupigiwa kelele za mwizi wananchi walikuja kuona nani mwizi wakiwa na silaha, walimkuta mzee fisi ndo mwizi watu wote walishangaa walimpa muda ajielezee kwanini kaiba. Mzee fisi alisema mimi sijaiba lakini nimekula chakula hapa hotelini sikuwa na hela ya kulipa, watu wote walishangaa sana wakasema mzee fisi acha utani tutakuuwa wewe na Mali zako zote hizo unakosa hela ya kulipa? Mzee fisi akasema jamani Mimi sina chochote mpaka saivi sina pakuishi watu wote waliguna mmh mmh mmh, wakauliza Mali zote hizo umepeleka wapi? Mzee fisi akasema Mimi nilikuwa na utajiri usio wa halali nulimtoa kafara mtoto wangu na Mali zangu zote zimeteketea kwa moto. Watu wote walikaa kimya kwa mda ghafla wakasikia sauti ikisema mzee fisi nilikwambia utajiri wako sio wa halali hivo basi maisha yako yatakuwa magumu sana.
Baada ya watu kusikia sauti hiyo wakamuuliza mzee fisi kumbe mzee fisi ulimtoa kafara mtoto wako ili upate utajiri.
Mzee fisi alijikuta akitoa nachozi huku akisema nilimtoa kafara mtoto wangu nili nipate utajiri lakini sikujua kama itakuwa hivi, na haya yote mganga wangu ndiye Aliniambia ili niupate utajiri inabidi nimtoe kafara mtoto wangu.
Watu wakauliza huyo mganga Yuko wapi? Mzee fisi akasema mganga wangu ameshafariki ilibidi watu wote wafikirie nini chakufanya.
Walipokuwa wakifikiria alipita baba mmoja akasema huyu mzee fisi hafai kwenye jamii yetu kwasababu ni mchawi huwa anatoa kafara watu nili apate utajiri ashamtoa mtoto wake. Watu baada yakusikia hayo walipata hasira sana wakaanza kumpiga mzee fisi, ghafla likapita gari la polisi katika eneo lile watu wote walikimbia polisi nao walishuka kwenye gari nakwenda kuangalia walipofika walimkuta mzee fisi amepigwa sana.
Polisi walimbeba mpaka kwenye kituoni walipomfikisha walianza kumhoji, mzee fisi unamatatizo gani? Mzee fisi akasema Mimi nimepigwa na wananchi kwa kosa lakula chakula hotelini nakushindwa kulipa, mama mwenye hoteli akanipigia kelele za kuwa Mimi ni mwizi na watu wakaja wakaanza kunipiga.............. Inaendelea.
JE POLISI WALICHUKUA HATUA GANI JUU YA MZEE FISI?
USIKOSE SEHEMU YA 6. YA UTAJIRI WA MZEE FISI.
Mwandishi: James P. Gerald.
Mawasiliani: 0767472566.
No comments:
Post a Comment