Breaking




Wednesday, 2 August 2017

MAANDALIZI YA KUMPOKEA MAGUFULI TANGA YAPAMBA MOTO

.

Maandalizi ya kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Magufuli katika mkoa wa Tanga yamezidi kupamba  moto katika maeneo mbali mbali ya mkoa huo.

Tovuti ya WW.DARMPYA.COM,iliweza kubahatika kupata picha zinazoonesha jinsi zoezi hilo linavyoendelea ambapo katika eneo la njia panda Segera kwa kumshudia Afisa Michezo jiji la Tanga Bwana Norbeth Paul Achiula akisimamia uwekaji wa mabango ya kukarabisha ugeni huo mkubwa katika  mkoa huo wa Tanga.

Rais Magufuli anatarajia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi linalojengwa katika eneo la Chongoleani Mkoani Tanga hadi Hoima mkoani Uganda. Bomba hilo la mafuta linatarajiwa kukuza uchumi wa mkoa wa Tanga na kuzalisha ajira zaidi ya 10,000.

No comments:

Post a Comment