Breaking




Sunday, 17 September 2017

MAYANJA AZUNGUMZIA UBINGWA, ATAMBIA SAFU YAO YA ULINZI

Sungo blog

Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja, amesema ushindi walioupata dhidi ya Mwadui unazidi kuwahahikishia nafasi ya wao kutwaa ubingwa msimu huu.

Pia aliipongeza safu ya ulinzi ambayo hadi sasa haijaruhusu bao hata moja na kuweka wazi kuwa hakuna timu ya kuwazuia wao kutwaa ubingwa msimu huu.

“Safu ya Ulinzi inabidi ipewe Hongera zake kwasababu mpaka hivi sasa hawajaruhusu bao, washambuliaji wengine wanashinda hivyo kwa kasi hii nazani hakuna wa kutuzuia sisi kupata ubingwa,” – Mayanja.

Akizungumzia sare waliyoipata wapinzani wao Yanga kwamba wameanza kujitoa katika mbio za Ubingwa, alisema hawezi kufurahia hilo kwani ligi ina timu 16 na zote zinahitaji ubingwa hivyo wao wanapambana na timu yao kwanza bila kuangalia timu nyingine zinapata matokeo gani.

Ligi ina timu 16 na kila timu inatafuta ubingwa, hata ukiangalia Mtibwa anaongoza huenda naye anaweza kuwa bingwa hivyo hatuangalii timu moja tunaangalia timu zote zinazoshiriki ligi kwa kupata ushindi,”.

Mayanja aliongeza, mchezo wao unaofuata dhidi ya Mbao anajua kiwa utakuwa mgumu kutokana na timu ya Mbao kupoteza michezo miwili mfululizo, lakini amedai hakuwapi presha kwani wanaamini watashinda.

No comments:

Post a Comment