Breaking




Sunday, 17 September 2017

RC MWANZA AMPA ULAJI MWALIMU HUYU.

Sungo blog

Umesha wahi kuusikia au kuutumia ule msemo wa ‘UALIMU ni wito’? Msemo huu  ni moja ya misemo mashuhuri sana katika jamii ya Kitanzania ikiwa na maana kuwa suala la kufundisha ni jambo linalofanywa kutoka moyoni kwa mtu ili kuifanya kazi hiyo kwa namna ya kufanikisha maendeleo ya mwanafunzi na kuinua ufaulu na uelewa.

Kauli hii imejidhihirisha baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella katika ziara yake ya kukagua shughuli maendeleo katika Wilaya ya Ukerewe kufanikiwa pia kutembelea Shule ya Sekondari Pius Msekwa.

Akiwa shuleni hapo RC Mongella alikutana na Mwalimu Obadia Obedi anayejitolea kufundisha masomo ya Sayansi Kidato cha Tano na kuagiza maombi yake ya ajira yafanywe haraka ili apate ajira ya kudumu.

No comments:

Post a Comment