Breaking




Thursday, 21 December 2017

MVUA KUBWA YA UPEPO YASABABISHA MAAFA MKOANI SHINYANGA

Sungo blog


Mvua kubwa ya upepo mkali imesababisha maafa katika vijiji vya Ukenyenge na Negezi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambapo imeezua paa za nyumba 37 pamoja na majengo Serikali.

Tukio hilo lilitokea saa 12 jioni ambapo majengo yaliyopatwa na maafa hayo ni ya pamoja na ofisi ya tarafa ya Negezi, ofisi ya afisa kilimo, ofisi ya TCRS.

Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Sahadrack Kengese alitembelea eneo hilo yalipotokea maafa akiwa amembatana na wataalamu kutoka halmashauri kwa ajili ya kufanya tathimini ya tukio hilo.

Mratibu wa Maafa Wilaya, Ponsian Kuhabwa na Mwesiga Katunzi kutoka Idara ya Ujenzi waliungana na viongozi wa tarafa na kata na kufanya tathimini hiyo ambapo bado hasara iliyotokea haijafahamika.

Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa Tarafa, David Isanga mara baada ya tukio hilo uongozi wa tarafa na kata ulishirikiana na wananchi kuhakikisha wanawasaidia wenzao walioathirika ili kurudisha hali.

Tathimini inaonesha kuwa hali ya maafa sio ya kutisha na ipo katika uwezo wa jamii kusaidiana na kuwa katika jengo la tarafa inaonyesha mahitaji mbalimbali ili kulirudisha katika matumizi.

Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa ni pamoja na ukarabati kufanyika haraka ili watumishi wapate sehemu za kufanyia kazi kwani sasa hivi wanabanana katika vyumba viwili vilivyosalimika.

Aidha, timu ya tathmini ilishauri kuendelea kupanda miti mbele ya jengo hilo ili kupunguza kasi ya upepo na kutunza mazingira katika eneo hilo. Pia wananchi wameshauriwa kupanda miti na kujenga nyumba imara ambazo zitasitahimili mitikisiko ya matukio kama haya.

No comments:

Post a Comment