Breaking




Wednesday, 20 December 2017

SHIRIKA LAPOSTA LAZINDUA NEMBO (LOGO) MPYA


Sungo blog

NEMBO MPYA

Shirika la posta la Tanzania leo limezindua nembo mpya na kuachana na nembo  ya zamani ambayo imetumika kwa takribani miaka 24 tangu pale mwaka 1994 ambaposhirikala posta lilianzishwa nchini. Nembo hiyo mpya mpya imeanza kutumika leo Rasmi.
 

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi alikuwaNaibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Mh. Elias Kwandikwa.Licha ya kuzindua nembo hiyompya,Wziri Kwandikwa pia alizindua magari manne mapya ya shirika hilo  kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na nyaraka mbali mbali ambazo zitakuwa zinasambazwa kwa kutumia njia ya posta.

 

Mh. kwandikwa amewataka Shirika la posta kuongeza ufanisi  katika utendaji kazi wao.

No comments:

Post a Comment