Breaking




Monday 26 June 2017

Bakwata yalaani mauaji Kibiti

ing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bakwata yalaani mauaji Kibiti

figganiggaJF-Expert Member

#1Today at 12:39 PM

Kwa ufupi
Sherehe hizo za Sikukuu ya Eid zimehudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye ndiye mgeni rasmi.By Emmanuel Mtengwa, Mwananchi
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Salumu Ahmed Abeid amesema baraza hilo linalaani mauaji yaliyotokea hivi karibuni wilayani Kibiti, mkoani Pwani.

Pia, Abeid amesema Bakwata imesikitishwa na vitendo hivyo vya mauaji kwa sababu vinachafua amani ya nchi.

‘’Baraza Kuu la Waislamu Tanzania linatoa pole kwa wananchi na limesikitiswa na vitendo vinavyotaka kuchafua amani ya nchi hasa vinapohusishwa na Uislam,’’ amesema Abeid leo, Jumatatu wakati akitoa salamu za Bakwata Taifa katika Bazaza la Eid mjini Moshi.

Kutokana hilo Bakwata imeiomba Serikali iongeze umakini katika kushughulikia suala la mauaji mkoani Pwani.

Swala ya Eid na Baraza la Eid, zinazofanyika kitaifa katika msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Sherehe hizo za Sikukuu ya Eid zimehudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye ndiye mgeni rasmi.

Wageni wengine ni pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira.


No comments:

Post a Comment