Breaking




Sunday 2 July 2017

BORESHA MAISHA NA TREND SOLAR, WATOA OFA KWA WATEJA NDANI YA SABASABA

Watanzania wameshahuriwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya kuboresha maisha  yao kwa kutumia Trend Solar za kisasa zenye ubora wa hali ya juu zilizoboreshwa sambamba na simu ya kisasa ya Smartphone, Solar paneli ya 20W,Chaja aina ya USB, Betri smati ya Sola, Tochi ya kuchaji,Taa 3 aina ya LED na mishikio ambazo unaweza kutumia chumbani, sebureni na nje ya nyumba yako ambapo kwa vyote hivyo vikipatikana kwa jumla ya Tsh. 531,000.
Trend Solar ambao wapo katika mabanda ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam wametoa ofa kabambe ya mteja kulipia kidogo kidogo kwa muda wa Mwaka mmoja.
“Boresha maisha kwa kulipia polepole. Kwa kianzio cha Tsh.93,000 tu! Baada ya hapo utachagua muda wa malipo ya aina mbili, kuna malipo ya wiki ambayo unaweza kulipa Tsh.8,423 ( kwa kila wiki) au ukaweza kulipa Tsh.36,500 malipo ya mwezi.  Hivyo jumla ya malipo ya  mwaka mmoja ni Tsh.531,000″. Alieleza Mtendaji Mkuu wa Trend Solar, Irfan Mirza.
Irfan ameongeza kuwa, Trend Solar ni sola za kisasa na zimekidhi viwango hivyo bidhaa hizo ambazo kwa sasa zimetokea kupendwa watu mbalimbali wamejitokeza kuzinunua na kuboresha maisha yao kwa nyumba zao kupata mwangaza wa taa, kupata mawasiliano ya kisasa ya simu ya smati trend solar ambayo inauwezo mkubwa wa kupiga picha, kuchati, kupakua App mbalimbali na mambo mengine.
Trend Solar wapo nje ya banda la Halotel ama jirani na hema la Mikumi ndani ya viwanja hivyo vya Sabasaba. Pia waweza kuwasiliana nao kwa kupiga simu ya bure bila malipo :0800713333 au kutembelea katika ofisi zao zilizopo jingo la RITA Tower 9th Floor lililopo mtaa wa Simu/Makunganya.
Mifumo yote inakuja kwa warantii ya miaka  2 katika betri smati ya sola na vifaa vingine kama vile balbu, simu, sola peneli na vingine vina warantii ya mwaka 1.
Waweza kutembelea mtandao wao kwa taarifa zaidi: http://boreshamaisha.com/
Imeandaliwa na Andrew Chale-MO BLOG,Sabasaba
Trend Solar kama zinavyoonekana pichani katika banda lao la Sabasaba
Wateja wakipewa maelezo namna ya bidhaa hizo za Trend Solar
Vifaa vinavyopatikana katika Trend Solar
Bi Natalie wa Trend Solar akiwa na smati ya Trend Solar ambayo ni moja ya simu mteja anapata kutoka katika bidhaa hizo.
Maafisa wakuu wa Trend Solar wakionesha betri smati ya Sola, kulia ni Arfan Mirza na kushoto ni Matt Tam
Bidhaa hizo za Trend Solar
20W Sola paneli
Mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa habari wa MO Blog,  Andrew Chale akipata maelezo juu ya bidhaa hizo za Trend Solar katika viwanja hivyo vya Sabasaba  yanayoendelea katika Barabara ya Kilwa.

No comments:

Post a Comment