Breaking




Sunday 2 July 2017

TANESCO YATUPIWA LAWAMA NA WANANCHI WILAYANI SENGEREMA

Wananchi wilayani Sengerema wamelilalamikia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilayani Sengerema kwa kukatika umeme mara kwa mara bila kutoa taarifa kwa umma.
Wananchi hao wametoa malalamiko hayo katika mahojiano na MO Blog ambapo wamedai kuwa umeme umekuwa ukikatika na kusababisha hasara kubwa ikiwemo kuunguza vifaa vya umeme na kusimamisha  shughuli zao kwa muda mrefu bila wahusika kuwajibishwa.     
Wameeleza kuwa idara husika kukata huduma ya umeme na kuendelea kukaa kimya bila kutoa taarifa kwa wananchi sio suluhisho la kudumu badala yake wanatakiwa watoe taarifa kwa umma ili kuepusha mkanganyiko kwa wananchi na kutupiwa lawama za mara kwa mara. 
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco wilayani Sengerema Samwel Mkumbo amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kudai kuwa changamoto kubwa inayosababisha hali hiyo ni ubovu wa miundombinu huku akiahidi  kutatua kero hiyo.
Tatizo la kukatika umeme mara  kwa mara wilayani Sengerema limedumu kwa muda mrefu sasa bila kupatiwa ufumbuzi na idara husika.

No comments:

Post a Comment