Kampuni ya huduma ya usafiri ya Uber inayofanya shughuli zake jijini Dar es Salaam imewakaribisha watu mbalimbali kujitokeza kujitokeza kuunganishwa na huduma hiyo ambayo imeweza kurahisisha maisha ya watu wengi kupitia usafiri ambapo mteja atakayepakua program ya Uber atapata ofa hiyo ya bure kwa safari ya kwanza.
Uber wapo nje ya banda la Wizara ya fedha na jirani ya banda la Karume katika mabanda ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam wametoa ofa hiyo kabambe ya mteja kuweza kuipakua App hiyo ya Uber kwa simu yake.
Kwa mujibu wa wataalam wa kampuni hiyo wameeleza kuwa, wateja wao wanaotembelea hapo watapata elimu mbalimbali pamoja na kufafanuliwa masuala ya kitaalam huku pia wakipata kuelekezwa namna ya kupakua program hiyo ya Uber yenye ofa ya punguzo la Tsh. 8,200 kwa safari ya kwanza.
“Uber kwa kipindi hiki cha Sabasaba tuna ofa maalum ya punguzo la Tsh 8,200, kwa mteja atakayejiunga sasa hivyo pesa hizo zinalipia safari yake ya kwanza. Mfano umei Uber ikupeleke sehemu ambayo ulitakiwa ulipe Ths 6,000, hapo hautolipa pesa utaenda bure. Pia kama utakuwa umeita Uber ukataka ikupeleke kwenye umbali ambao ungetakiwa kulipa Tsh. 12,000, hapo utalipa 4,000 pekee hii ni kwa wateja ambao watakuwa wamejiunga na ofa yetu” ameeleza Alfred Msemo kutoka Uber.
Uber kwa Jiji la Dar es salaam imeelezwa kuwa ni miongoni mwa jiji la 475 duniani kujiunga na mtandao huo ambao unatoa huduma ya usafiri katika majiji mbambali duniani.
Huduma ya mtandao wa Uber, huwaunganisha madereva na wasafiri kwa muda muafaka, kwa kubonyeza tu kitufe cha Uber na kuagiza usafiri ambapo gari inakufuata mahala ulipoielekeza.
Tazama hapa kuona tukio hilo:
Geoffrey Mabula wa Uber akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotembelea banda hilo
Davis Evans wa Uber akimpatia maelezo ya namna ya kupakua programu ya Uber kwa mteja aliyetembelea banda hilo
Geoffrey Mabula wa Uber akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotembelea banda hilo
Francis Kimario wa Uber akitoa maelezo kwa wateja waliopita katika banda hilo la Uber
Josephine Juma wa Uber akiwa na tuzo ya ubora walioshinda katika maonesho hayo ya Sabasaba
Geoffrey Mabula wa Uber akiwa na tuzo walioshinda katika maonesho hayo ya sabasaba
Geoffrey Mabula wa Uber akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotembelea banda hilo
Monica Mziray wa Uber akitoa ufafanuzi wa wananchi waliofika katika banda hilo
Tuzo ya Uber
Timu ya Uber ikiwa katika viwanja hivyo vya Sabasaba mwaka huu tayari kwa kukusaidia namna ya kutumia huduma ya usafiri wa Uber. ( Picha zote na Andrew Chale)
No comments:
Post a Comment