Breaking




Sunday 2 July 2017

Global Education Link Ltd yapata tuzo Maonesho ya Sabasaba 2017

Kampuni ya Global Education Link Ltd imekabidhiwa Ngao ya Ushindi na RaisMagufuli ikiwa ni ishara ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje‘TanTrade’ kutambua mchango wa kampuni hiyo kudhamini maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwa siku 14.
Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Maonesho ya Sabasaba yamefunguliwa rasmi July 1, 2017 na Rais Magufuli ambapo hufanyika kila mwaka katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Kilwa Road DSM yakiambatana na utoaji tuzo mbalimbali kwa makapuni washiriki.
Aidha, wakati wa ufunguzi huo Rais Magufuli alitembelea Banda la Global Education link Ltd na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kudahili Wanafunzi.
Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link Ltd Bi. Zakia Nassor (kushoto) akipokea Ngao ya Ushindi kutoka kwa Rais Magufuli. Anayeshuhudia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage
Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link Ltd Bi. Zakia Nassor (kushoto) akipewa pongezi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage
Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link Ltd Bi. Zakia Nassor (kushoto) akipewa pongezi na Rais Magufuli huku Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Mwenyekiti wa Bodi ya TanTrade Eng. Christopher Chiza wakishuhudia

No comments:

Post a Comment