Breaking




Saturday 1 July 2017

UBINGWA


 Timu ya Storaway FC imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Three boys cup baada ya kuikung'uta Vijuso FC mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Halmashauri ya wilaya Liwale mkoani Lindi.

 Mchezo huo wa fainali uliochezwa leo juni 30 ulianza kwa kasi kwa kila timu ilionekana kuwa na shauku ya kupata bao. Storaway fc ilianza kufungua kalamu ya mabao baada ya kufunga bao la kuongoza namo dakika ya 19 na bao la pili lilifungwa  dakika ya 37 na mpaka mapumziko Vijuso hawakupata goli.

 Katika kipindi cha pili Mchezo uliendelea kuchezwa kwa kasi kwa kila timu ikisaka magoli lakini namo dakika ya 85 timu ya Storaway iliweza kuandika S goli la tatu na goli hilo lilidumu mpaka dakika 90 zinakamilika na matokeo kuwa Storaway 3 na Vijuso fc bila.

 Zawaidi zilizotolewa kwa washindi leo ilikuwa kama ifuatavy,Timu ya Storaway fc ambao ndio mabingwa wa ligi ya Three boys cup waliweza kupewa fedha shilingi laki saba (700,000) na washindi wa pili ambao Vijuso fc waliweza kuzawadiwa shilingi laki tatu (300,000). 

No comments:

Post a Comment