Said Mohamedi golikipa namba mbili wa timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars amechaguliwa kuwa kipa bora wa michuano ya COSAFA mwaka iliyokuwa ikipigwa huko Afrika kusini.
Said amepata nafasi hiyo ni baada ya kucheza mechi moja tu kwenye michuano hiyo,mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Lesotho ambapo Tanzania walipata ushindi kwa njia yaq penaiti 4-3 na kuchukua ushindi wa tatu wa michuano hiyo.
Katika mchezo huo Said alionekana kuwa shujaa kwa kuokoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa Lesotho na baadae aliweza kuokoa penaiti .







No comments:
Post a Comment