Taharuki imetokea kwa wananchi wa Kimara Baruti jijini Dar es salaam baada ya dada mmoja aliyejulikana kwa jina la Zuena Mapunda kudai kauziwa mchele usioleweka ambao unasemekana ni wa plastiki kama ambavyo taarifa za uwepo wa mchele huo zinavyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza na Channel Ten Zuena Mapunda amedai kununua mchele huo kilo 100 juzi kwa ajili kutumia msibani ambapo amesema walianza kuupika kwa muda mrefu bila kuiva jambo lililowatia hofu kutokana na taarifaza kuwepo mchele bandia ,hivyo kuamua kuufinyanga na kuudunda chini bila kuvurugika na kubaini kuwa haukuwa wa kawaida,ndipo walipoamua kuurudisha.
Sakata hilo limekusanya wengi waliokuja kushuhudia mchele huo huku maelewano yakikosekana baina ya muuzaji na mnunuz,i licha ya awali mmiliki wa duka hilo kukubali kupokea mchele huo na kumrudishia fedha zake.
Hata hivyo baada ya Muda walifika askari pamoja na afisa afya kutoka manispaa ya ubungo na kuingilia kati licha ya pande hizo mbili kushindwa kuelewana ambapo iliamuliwa kuchukuliwa kwa sampuli kwa ajili ya kupeleka kwa mamlaka husika ili kujiridhisha endapo tuhuma hizo ni za kweli.
Katika hali ya kushangaza baada ya kumalizika kwa taratibu zote na kumtaka mmiliki wa duka kuhifadhi ndani mchele uliokuwa umezuiwa mlangoni akikataa na kuwataka waondoke nao licha ya kuwarudishia fedha jambo ambalo lilileta utata na kuamua upelekwe serikali za mtaa wa kimara Baruti mpaka vipimo vitakapokamilika.
VIDEO:WATU WATATU WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA AJALI HUKO IRINGA







No comments:
Post a Comment