Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke jijini Dsm limeanzisha Operesheni ya nyumba kwa nyumba,Mtaa kwa mtaa wilayani temeke kwa kuwashirikisha wenyeviti wa kamati za usalama za mitaa kufuatia kubaini baadhi ya watuhumiwa wa uhalifu katika eneo hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Giles Muroto akizungumza na wenyeviti wa mitaa na watendaji amesema baadhi ya watuhumiwa wamekuwa wakijificha wilayani humo ili kukimbia msako wa jeshi hilo unaoendelea Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.
Aidha, Kamanda Muroto ametangaza Operesheni ya kuwasaka watoto watoro mashuleni wilayani Temeke itakayowashirikisha wenyeviti wa mitaa, ikiwemo wale wasioonekana kwa wazazi wao ambao inadaiwa zaidi ya watoto 1400 hawaonekani shuleni au kwa wazazi wao, hali inayotia mashaka ya kujiunga na makundi yasiyofaa.
VIDEO:UONGOZI WA SIMBA WABARIKI SAID NDEMLA KWENDA NCHINI SWEEDEN








No comments:
Post a Comment