Kukamatwa kwa Mbunge wa upinzani nchini Tanzania Halima Mdee kwa madai ya kumtusi Rais John Magufuli kumeshutumiwa pakubwa huku wakosoaji wakisema kuwa ni ishara ya hivi karibuni kwamba serikali inatumia mamlaka yake vibaya ili kukandamiza uhuru wa kujieleza.
Msemaji wa chama cha upinzani CHADEMA, Tumaini Makene ameambia BBC kwamba chama hicho kitakwenda mahakamani dhidi ya hatua ya mkuu wa Wilaya ambae aliagiza kukamatwa kwake pamoja na makamishna wengine wote wanaokiuka sheria.
Bi Mdee ni mwanachama wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani katika Taifa hilo la Afrika Mashariki akipanda gari la polisi
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee aliyewekwa rumande kwa amri ya Mkuu wa Wilaya
Alituhumiwa na Ally Hapi, mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kumtusi Rais na kuchochea ghasia baada ya kudai kwamba Rais anafikiri kwamba matamshi yake ni Sheria na kwamba siku moja atawaagiza Watanzania kukaa utupu.
Muungano wa mabadiliko na uwazi unaongozwa na Zitto Kabwe ulisema kuwa hatua hiyo ni uendelevu wa utumiaji mbaya wa mamlaka.
”Sheria inayompatia mkuu huyo wa Wilaya uwezo wa kuagiza kukamatwa kwa mtu, hailingani na sababu ya kukamatwa kwa bi Mdee,” alisema.
Watu kadhaa wamekamatwa katika siku za nyuma kwa kuchapisha ujumbe katika mitandao ya kijamii ambayo mamlaka inadai inaingilia kisiasa.
Mamlaka inaamini kwamba inafuata sheria na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba hakuna ”migogoro yoyote miongoni mwa wananchi” nchini Tanzania.
Bwana Magufuli alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka 2015 na licha ya kukosolewa na upinzani pamoja na makundi ya wanaharakati anaungwa mkono na Watanzania wengi.
HT @ BBC Swahili
No comments:
Post a Comment