Breaking




Tuesday, 25 July 2017

WAZIRI MKUU ASHUTUMIWA KWA UPENDELEO





Tokyo, Japan. Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe ametupilia mbali shutuma zilizoelekezwa kwamba alitumia vibaya ushawishi wake akamsaidia rafiki yake kufungua shule ya mafunzo ya mifugo.

Kashfa hiyo ya upendeleo imezidi kumuweka pabaya hadi kushusha umaarufu wake.

Kwa msaada wa viwango vipya vya Baraza la Mawaziri lililochafuka kwa kashfa, Abe amehojiwa tena leo Jumanne na Bunge la Juu kuhusu madai kwamba aliingilia kati ili kumsaidia rafiki yake kupata idhini ya kufungua shule ya mafunzo ya mifugo Magharibi mwa Japan.

Katika utetezi wake, Abe aliwaambia wabunge hao kwamba hakuwahi kuombwa na rafiki amsaidie apewe uthibitisho kwa ajili ya kufungua shule katika Jiji la Imabari, Kusini Magharibi mwa Kisiwa cha Shikoku.

Jana Jumatatu, Abe alikanusha shutuma hizo katika kikao cha Bunge la Chini. Abe alisema rafiki yake Kotaro Kake hakuwahi kuomba msaada na wala yeye hakuwahi kumsaidia katika suala la kuanzishwa kwa shule inayotajwa.

"Napenda kuweka wazi kwamba (Kake) hakuwahi kunitaja wala kuomba ushauri kuhusiana na shule ya mafunzo,” alisema Abe.

No comments:

Post a Comment