Breaking




Sunday, 13 August 2017

ALICHOZUNGUMZA ALLY MAYAY TEMBELE BAADA YA KUKOSA URAIS WA TFF



Aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mayay ametoa ya moyoni kuhusu uchaguzi huo uliofanyika jana Jumamosi kwenye Ukumbi wa St Gasper mjini Dodoma.

Baada ya kumalizika kwa mchakato huo wauchaguzi uliosimamiwa na kamati ya uchaguzi chini ya Wakali Revocatus Kuuli, mgombea Mayay alifunguka na kusema "Hii ndiyo maana ya demokrasia au ambayo Fifa na CAF wanaizungumzia kila siku. Uchaguzi ulikuwa wa huru na haki na hata walioshinda walipata nafasi hiyo kwa uhalali," alisema.

"Sikufanikiwa kupata nafasi kwani kura zangu hazikutosha ila ninachoomba washindi waliopata nafasi hiyo kuendeleza soka na kuyatimiza yale ambayo waliahidi wakati wa kampeni," alisema Mayay.

Uchaguzi huo ulimalizika na Wallece Karia kuwa ndiye Rais na Michael Wambura kuwa makamu huku wakipatikana wagombea wengine 13, kutoka katika kila kanda.

No comments:

Post a Comment