Sungo blog
Msemaji machachari wa klabu ya Ruvu Shooting,Masau Bwire amesema ushindi walioupata Simba wa goli 7-0 dhidi ya timu yake ya Ruvu Shooting leo ni miujiza.
Masau Bwire ameyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha michezo cha E-spots kinachorushwa na EFM.
Maasau amesema ushindi waliopata simba ni miujiza kama miujiza mingine ambayo mwezimungu anaamua kuileta,na sio uwezo wa Simba.
"Ile ni miujiza tu kama ilivo mingine, hakuna goli lolote la kiufundi ambalo simba wamefunga" Aliseme Masau Bwire
Simba wameifunga Ruvu shooting magoli saba kwa sifuri ,magoli yaliyofungwa na Emannuel okwi(4),Kichuya (1),Erasto Nyoni (1) na Juma Luizio (1)






No comments:
Post a Comment