Breaking




Saturday, 26 August 2017

MAN CITY,NEW CASTLE NA SWANSEA ZASHINDA

Sungo blog


                         

Ligi kuu ya England imeingia katika mzunguko wa Tatu leo kwa mechi 5 kuchezwa tayari huku mechi moja baina ya Manchester United dhidi ya Leicester City ikiendelea .

Manchester City iliweza kuifunga AFC Bournemouth bao 2-1 katika mchezo ulikokuwa mkali huku Man City wakisawazisha bao na kuongeza bao la ushindi dakika za Mwisho kabisa likifungwa na Raheem Sterling.

Newcastle United ikafanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0 nyumbani dhidi ya West Ham United katika mchezo uliopigwa katika dimba la St. James Park ukiwa pia ndiyo ushindi wa kwanza Newcastle msimu huu.

Matokeo mengine Crystal Palace ikiwa nyumbani imefungwa bao 2-0 na Swansea hali ikiendelea kuwa mbaya kwa kocha mpya wa Palace Frank De Boer.

Wageni katika ligi Brighton wakiwa ugenini wameweza kupata sare ya bila kufungana na Watford matokeo kama hayo yakiwafika pia Huddersfield Town waliokua nyumbani wakicheza dhidi ya Southampton.

No comments:

Post a Comment