Breaking




Saturday, 26 August 2017

WACHEZAJI 21 WA TAIFA STARS WALIOITWA NA KOCHA LEO

Sungo blog

Kocha.wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa.stars ,Salum Mayanga leo Agost 26 ametaja kikosi cha wachezaji 21 watakaoingia kambini kujiandaa na.mchezo dhidi ya Botswana mchezo utaokaochezwa Sptemba 2,2017.

Mchezo huo ni wa kirafiki wa wiki ya FIFA ambapo wachezaji walioitwa wataingia kambini kesho saa 2 usiku tayari kwa maandalizi ya mechi hiyo itakayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru Jumamosi ijayo.

Kikosi kamili kilichotangazwa na Kocha Mayanga ni magolikipa Aishi Manula, Mwadin na Ramadhan Kabwili.

Walinzi ni Gadiel Michael, Boniface Maganga, Abdi Banda, Yondan, Salim Mbonde na Erasto Nyoni. Viungo ni Himid Mao, Hamis Abdallah, Mzamiru Yasin na Said Ndemla.

Mawinga ni Simon Msuva, Shiza Kichuya, Farid Mussa na Molel Ergenes wakati washambuliaji ni Mbwana Samata, Elius Maguri, Kelvin Sabato na Raphael Daud.


No comments:

Post a Comment