Mbunge wa Singida Mashariki ambaei pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, amekamatwa na jeshi la polisi leo alipokuwa anatoka mahakamani Kisutu .
Taarifa zinasema amekamatwa kwa ajili ya mahojiano.
"Tumetoka Mahakama ya Kisutu muda huu ambapo Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lissu alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi (uchochezi one) lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili Yericko Nyerere hapa hapa Kisutu."
"Wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likawa blocked na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police."
"Wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Police". Amesema Makene.
Taarifa zaidi tutakuletea hapo badae







No comments:
Post a Comment