Breaking




Sunday, 6 August 2017

JAMAA ANUSURIKA KICHAPO BAADA YA KUCHANGISHA RAMBIRAMBI YA UTAPELI




 

Kuna msemo usemao Ugumu wa Maisha ni kipimo cha Akili, au kuishi Bongo kunahitaji kutumia bongo.

Hayo yamemkuta kijana mmoja katika mtaa wa Mpakani kijitonyama jijini Dar es salaam, aliyejitambulisha kwa jina la Hamza Joseph ambaye inadaiwa aliamua kuwachangisha pesa za kugharamia msiba wa aliedai ni mdogo wake wa miaka miwili ambaye amefariki, huku ikielezwa kuwa hakuna msiba wala kijana huyo hajulikani mtaani hapo.

Hatua hiyo ililazimu wakazi hao kuamua kumuweka chini ya ulinzi wakitishia kumpatia kichapo kwa kufanya utapeli.

No comments:

Post a Comment