Joto la uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) limezidi kupanda mkoani Dodoma huku wagombea na wadau mbalimbali wakiuzungumzia kwa mitazamo tofauti.
Baadhi ya wadau wameutaja kuwa ni uchaguzi mgumu tofauti na zilizopita huku baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali wakiahidi kufanya mabadiliko ndani ya shirikisho hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wagombea hao wamesema kuwa TFF inahitaji mabadiliko ya kiutendaji ambayo yanakwenda sambamba na ulimwengu.
Nao wapiga kura ambao ni wajumbe wa mkutano huo, wamewataka wenzao kuacha kupiga kura kwa mazoea na badala yake waangalie zaidi maslahi ya watanzania zaidi ya milioni 40 ambao wanapenda mchezo wa mpira wa miguu.
Wakati wagombea wakiendelea kujinadi katika dakika za majeruhi za kampeni, afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amerejeshwa jijini Dar es Salaam kutoka Dodoma kwa tuhuma za kumpigia kampeni mgombea mmojawapo wa urais, Richard Shija.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mjini Dodoma kesho Agosti 12 ambapo wagombea pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF tayari wamewasili kwa kazi moja ya kushiriki zoezi hilo muhimuu kwa maendeleo ya soka nchini.
No comments:
Post a Comment