Breaking




Friday, 11 August 2017

TFF YATOLEA UFAFANUZI ISSUE YA ALFRD LUCAS


Baada ya headlines na taarifa za afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas kusambaa kuwa karudishwa Dar es Salaam kwa tetesi au tuhuma za kumpigia kampeni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais wa TFF Shija Richard.

Kaimu katibu Mkuu wa TFF Salum Madadi ametoa ufafanuzi huu kuhusiana na madai na taarifa hizo “Hapana hazina ukweli hakurudi kwa sababu hiyo Lucas amerudi Dar es Salaam kwa sababu tuna majukumu mengine tu lakini sio kwa sababu hiyo amemaliza shughuli zake na anarudi kwa majukumu mengine” Madadi

Kwa habari za chini ya kapeti zilizoenea Dodoma kutoka katika vyanzo vya kuaminika inadaiwa kuwa Alfred Lucas alisalimiana na mgombea Urais wa TFF Shija Richard kitendo ambacho kimedaiwa kusababisha viongozi wake wamrudishe Dar es Salaam kwa madai anampigia kampeni mgombea huyo.

No comments:

Post a Comment